Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela, akutana na Katibu Mkuu Kiongozi – 07 Machi, 2019


Mar 07, 2019

Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela, leo 07 Machi, 2019 amekutana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John W. H. Kijazi ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es salaam, ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha kwake toka aingie rasmi kazini hivi karibuni.

Katika ziara yake hiyo Bw. Nsekela aliambatana na Ndugu Ally H. Laay ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo pamoja na Bi. Tully Esther Mwambapa ambaye ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki hiyo.

Itakumbukwa kuwa mapema mwezi Oktoba mwaka 2018, ndugu Nsekela aliteuliwa kuwa mkurugenzi mtendaji mpya wa Benki hiyo, hivyo basi hii ni mara yake ya kwanza kukutana na kujitambulisha rasmi kwa kiongozi huyo mkuu wa Utumishi wa Umma nchini.